Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

SIKU 20 YA 30

Kama ilivyokuwa wakati wa kanisa la kwanza, leo pia tunakabiliana na wahubiri na waalimu wa uongo. Hawa wanajishughulisha zaidi na mambo yahusuyo heshima na utajiri wa ulimwengu huu. Lakinisisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo, anakumbusha Paulo (2:17). Mkazo mkuu wa wanaofundisha uongo ni kutaka kujinufaisha kwa njia ya mali, heshima na kujitwalia utukufu. Badala ya kujaa Roho Mtakatifu hujaa roho mtakavitu. Tunaweza kuwatambua hawa kwa njia ya kupima mafundisho na maisha yao. Neno la Mungu ndilo kipimo halisi.Bwana asema hivi, Mizoga ya watu itaanguka kama samadi juu ya mashamba, Na kama konzi ya ngano nyuma yake avunaye, wala hapana mtu atakayeikusanya. Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake(Yer 9:22-23). Unaweza pia kusoma Mt 7:15-23.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana