Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

SIKU 5 YA 31

Kwa kuwa Mungu alifahamu nia mbaya ya Mfalme Herode, alimtokea Yusufu kumwambia amchukue mtoto na wakimbilie Misri ili Herode asimwangamize katika hila yake. Yesu alizaliwa kwa kusudi maalumu la Mungu ili aokoe ulimwengu na dhambi. Yusufu alitii, akakaa Misri mpaka Herode alipokufa, sawa na unabii wa Hos 11:1,Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri. Hasira za Herode kwa kutokuweza kumwua mtoto Yesu, zilimfanya awaue watoto wote wa kiume wa miaka miwili kwenda chini. Alisababisha maafa makubwa yaliyosababisha maombolezo makuu,Sauti imesikiwa Rama, kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako(Yer 31:15).

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu ch...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha