Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

SIKU 31 YA 31

Tulijifunza katika somo la jana kwamba Daudi alitambua kuwa kimbilio liko kwa Bwana Mungu tu. Baada ya kutambua haya, Daudi aliendelea kumsifu Mungu kwa utukufu wa kazi yake kwa wanadamu. Kwa ujumla Zaburi ya 40 ni zaburi ya sifa na utukufu kwa Bwana kwa yale aliyotutendea. Ieleweke kwamba, anayemsifu Mungu si lazima aelezee raha anayoipata tu. Bali katika sifa zake anayo hata nafasi ya kumwambia Mungu yale yanayomkosesha amani:Mabaya yasiyohesabika Yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, Wala siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, Na moyo wangu umeniacha.
13 Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa, Ee Bwana, unisaidie hima
(m.12-13). Tuendelee kumsifu Mungu kwa kazi yake kwetu, tukiomba kama Daudi katika m.17:Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu ch...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha