Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

SIKU 8 YA 31

Yohana alitambua kuwa yeye ni mjumbe tu aliyetangulia, lakini yupo ajaye aliye mkuu zaidi. Yesu ndiye aliyekamilisha yale aliyoyaeleza Yohana. Yesu alinyenyekea anapokubali kubatizwa na Yohana. Lilikuwa tendo la kujitoa wakfu kwa kazi ya kumkomboa mwanadamu. Baada ya Yesu kubatizwa, ubatizo wa Kikristo ulianza ukiashiria mwanzo wa kipindi kipya cha wana wa Mungu. Katika m.16-17 tunaona utatu wa Mungu, Yesu akiwa Mwana, Roho Mtakatu kwa mfano wa hua, na Baba kwa njia ya sauti kutoka mbinguni:Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu ch...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha