Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Adui wa MoyoMfano

Enemies Of The Heart

SIKU 5 YA 5

Andy Stanley: Adui wa Moyo


Ibada ya Siku ya 5


“Kuchukua Shauu zako kwa Mungu”


Andiko: Yakobo 4:1-3


Kila adui wa moyo anasukumwa na dhana kwamba kuna mtu anayenidai kitu. Hatia inasema, “nina deni.” Hasira inachochewa na dhana kwamba unanidai. Tamaa inahuishwa na wazo kwamba ninajidai. Shida ya nne ya moyo si tofauti. Wivu. Wivu unasema, “Ninamdai Mungu.”


Tunapofikiria kuhusu wivu ama husuda, mara moja tunafikiria kuhusu vitu ambavyo watu wengine wanavyo ila tunakosa—urembo, maarifa, nafasi, afya, urefu, urithi, n.k. Tunadhani kwamba shida yetu ni ya mtu anayemiliki tunayokosa. Lakini tukubali; Mungu alikuwa na uwezo wa kuirekebisha kwa niaba yetu. Chochote alichompa jirani yako, angekupa wewe pia. Pengine ndio sababu unahisi ndani kwamba unamdai Mungu.


Wivu unaweza kutishia maisha yako na kusababisha madhara katika uhusiano wako. Habari njema ni kwamba, dubwana hili, kama matatu mengine, lina udhaifu. Na ni jambo ambalo hungetarajia: acha kutamani vya wengine na anza kumwomba Mungu akupe anavyojua ni bora zaidi kwako.


Kama Yakobo anavyosema, vita vyenu vya nje ni matokeo ya moja kwa moja ya vita vya ndani ambavyo vimeweza kujitokeza nje. Tunataka kitu lakini hatuna, kwa hivyo tunapigana na wengine. Shauku ambayo Yakobo anazungumzia katika kifungu hiki zinawakilisha kiu Isiyoweza kutoshelezwa—Shauku ya vitu, pesa, sifa, mafanikio, maendeleo, urafiki wa karibu, ngono, raha, uhusiano, ushirikiano.


Kwa hivyo tunafanya nini na tamaa na kiu ambazo hatimaye haziwezi kutoshelezwa kwa ukamilifu? Yakobo anasema tuzipeleke kwa yule ambaye aliziumba mwanzoni. Yaani, Yakobo anatupa ruhusa kufungua roho kusema na Muumba wetu katika mazungumzo yasiyosanifishwa.


Kila hitaji ulilonalo, kubwa au dogo, ni muhimu kwa Baba kwani wewe ni muhimu kwa Baba. Ikiwa inahusu maisha yako ya mapenzi, kazi yako, ndoa yako, wazazi wako, watoto wako, fedha zako, masomo yako, ama muonekano wako, mletee. Na endelea kumletea mpaka upate amani ya kuinuka kutoka kupiga magoti ili kukabiliana na siku, ukiwa na uhakika kwamba anakujali.


Ngoja nikuhakikishie kwamba moyo wako utabaki kuwa na thamani kuu kwake daima.


Moyo wako unaumia juu ya nini? Chukua muda kusema na Mungu katika mazungumzo yaliyo huru na yasiyozuilika kuhusu unachohisi unakosa. Mwombe akubariki kwa njia ambayo anajua ni bora zaidi—na adhihirishe upendo wake kwako


Tunatumai umefurahia ibada hii ya siku 5 ya Andy ya YouVersion kuhusu "Adui wa Moyo." Chukua kitabu cha Andy, Enemies of the Heart, kutoka duka lililo karibu nawe ili kuchunguza zaidi na kupata uponyaji na urejesho wa muda mrefu.


 


Andiko

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Enemies Of The Heart

Kama vile moyo unaougua unavyoweza kuangamiza mwili wako, moyo wa kihisia na kiroho unaougua unaweza kukuangamiza pamoja na mahusiano yako. Kwa siku tano zifuatazo, ruhusu Andy Stanley akusaidie kujitazama ndani yako adu...

More

Tungependa kuwashukuru Andy Stanley na Multnomah kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: bit.ly/2gNB92i

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha