Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Adui wa MoyoMfano

Enemies Of The Heart

SIKU 4 YA 5

Andy Stanley: Adui wa Moyo


Ibada ya Siku ya 4


“Kujihadhari na Tamaa”


Maandiko: Luka 12:13-21


Adui wa tatu wa moyo? Tamaa. Hii ni wakati ambapo tunahisi kuwa tunastahili kupata mali zaidi na zaidi. Tamaa inasema, “Ninajidai.”


Yesu alisema, “Jihadharini! Jilindeni na aina zote za choyo.” Mbona? Kwa sababu kutoka magonjwa manne ya moyo ambayo tunazungumzia, tamaa ni ngumu zaidi kutambua. Tamaa inaweza kuingia moyoni mwetu na kuishi pale kwa miaka na miaka bila kugunduliwa. Moyo usiokingwa u hatarini mno kwa ugonjwa huu unaoangamiza. Ni ngumu kugunduliwa—hasa kugundua mwenyewe kwamba upo moyoni mwako.


Yesu aliendelea na kufunua uongo unaochochea tamaa yote: “Maisha ya mtu hayatokani na wingi wa mali alizo nazo.” Lakini nani hajui hivyo? Kuna watu ambao kwa kweli wanaamini kwamba maisha yao ni sawa na wanachomiliki? Jibu ni hapana na ndiyo. Hapana, si kila mtu anajua hivyo. Na ndiyo, kuna watu ambao wanaamini kwamba maisha yako ni idadi ya jumla ya yote unayomiliki. Na wengi wetu leo tunaaweza kuathiriwa na imani hii kuliko tunavyofikiria.


Baada ya kutoa mfano, Yesu alitoa maana ya mtu mwenye tamaa: mtu anayejiwekea vitu lakini hajitajirishi kwa Mungu.“Kujitajirisha kwa Mungu” ni maneno Yesu anatumia kumaanisha kuwa mkarimu kwa wahitaji. Mtu mwenye tamaa ni yule anayehakikisha kwamba ameweka akiba lakini hataki kutoa.


Ukarimu utavunja ngome ya tamaa maishani mwako. Kwa hivyo ikiwa una la ziada ama huna, toa na utoe kwa ukarimu. Lazima utoe hadi unalazimika kubadilisha mtindo wako wa maisha. Ikiwa huko tayari kutoa hadi unalazimika kubadilisha mtindo wako wa maisha, basi kulingana na Yesu, una tamaa. Ikiwa unakula hadi huna chochote cha kutoa ama kidogo sana, una tamaa. Ikiwa unakula na kuhifadhi hadi huna chochote cha kutoa ama kidogo sana, una tamaa.


Najua hilo ni zito. Kwa kweli, ni ngumu.


Lakini ni ukweli.


Vunja nguvu ya tamaa kupitia tabia ya kutoa kwa ukarimu. Ni tabia inayobadilisha kila kitu.


Tathmini ukarimu wako wa kutoa katika mwaka uliopita. Utoaji wako unasema nini kuhusu moyo wako? Omba kuhusu vitu ambavyo ungependa kufanya katika mwaka ujao ili kuwa mkarimu zaidi.


siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Enemies Of The Heart

Kama vile moyo unaougua unavyoweza kuangamiza mwili wako, moyo wa kihisia na kiroho unaougua unaweza kukuangamiza pamoja na mahusiano yako. Kwa siku tano zifuatazo, ruhusu Andy Stanley akusaidie kujitazama ndani yako adu...

More

Tungependa kuwashukuru Andy Stanley na Multnomah kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: bit.ly/2gNB92i

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha