Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Adui wa MoyoMfano

Enemies Of The Heart

SIKU 1 YA 5

Andy Stanley: Adui wa Moyo


Ibada ya Siku ya 1


“Volkeno Inayoiga”


Maandiko: Mathayo 15:1-20


Mwelekeo wetu ni kufuatilia tabia zetu ilhali tunapuuza mioyo yetu. Hata hivyo, unafuatilia vipi moyo wako? Siwezi kupotoka sana katika tabia zangu bila mtu kunijulisha. Lakini moyo wangu? Huo unatatanisha.


Yesu alisema kitu ambacho kinaendelea kuwa na maana hata leo: “Kitokacho kinywani mwa mtu hutoka moyoni,” na kisha, “Ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya.”


Moyo ni fumbo kuu. Isitoshe, nabii mmoja alisema kuuhusu, “Ni nani awezaye kuujua?” (Yeremia 17:9). Swali nzuri. Maana ni kwamba hakuna aliye na uwezo huo. Na ninakubaliana na hayo. Na hata tukianza kuuelewa, hakika hatuwezi kuudhibiti—ambayo ni sababu nyingine ya kuufuatilia. Kama mtikisiko wa ndani wa volkeno, unajuaje yale ambayo yanaweza kukuumiza.


Ghafla mtu anaomba talaka.


Ghafla alama za mtoto zinapungua na mtazamo wake unabadilika.


Ghafla tafrija isiyo na madhara inakuwa tabia inayoangamiza.


Ghafla maneno makali yanachoma moyo wa mpendwa asiyetarajia.


Sote tumeona, hisi, hata kusababisha. Kama vile Yesu alivyotabiri, kinachotoka kwenye siri ya mioyo yetu hakitabaki siri kamwe. Hatimaye kitaingia nyumbani mwetu, ofisini, na mitaani.


Moyo unaingilia kila mazungumzo. Unaamua kila uhusiano. Maisha yetu yenyewe yanatokana na moyo. Tunaishi, tunalea watoto, tunaongoza, tunahusiana, tunachumbiana, tunakabili, tunaitikia, tunajibu, tunaagiza, tunasimamia, tunatatua shida, na kupenda kutoka moyo. Mioyo yetu inaathiri ukali wa mawasiliano yetu. Mioyo yetu ina tabia ya kuzidisha hisia zetu na usugu wetu. Kila sehemu ya maisha inaingiliana na kinachotendelea mioyoni mwetu. Kila kitu kinapitia njia kokote kinakoelekea. Kila kitu.


Tunahitaji ujasiri kumwomba Baba wa mbinguni atusaidie kuchunga, kuelewa, na kutakasa mioyo yetu. Ana hamu kuu kutujibu na kutuonyesha jinsi ya kubadili tabia mbaya za kale za moyo na tabia mpya na bora ambazo kwa wakati zitatufanya tuwe kama Mwana wake.


Katika siku nne zijazo za ibada hii, tutaangalia adui wanne wa moyo ambao kila mtu anakabiliana nao.


Fikra zako za hivi karibuni, maneno, na vitendo vinaashiria nini kuhusu yanayofanyika moyoni mwako? Mwulize mtu wa karibu akupe maoni yake pia.


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Enemies Of The Heart

Kama vile moyo unaougua unavyoweza kuangamiza mwili wako, moyo wa kihisia na kiroho unaougua unaweza kukuangamiza pamoja na mahusiano yako. Kwa siku tano zifuatazo, ruhusu Andy Stanley akusaidie kujitazama ndani yako adu...

More

Tungependa kuwashukuru Andy Stanley na Multnomah kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: bit.ly/2gNB92i

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha