Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Adui wa MoyoMfano

Enemies Of The Heart

SIKU 2 YA 5

Andy Stanley: Adui wa Moyo


Ibada ya Siku ya 2


“Ungama”


Maandiko: 1 Yohana 1:5-10


Adui wa kwanza wa moyo ni hatia. Hatia ni tokeo la kufanya kitu ambacho tunafikiri ni kosa. Ujumbe kutoka moyo wenye hatia ni, “nina deni!”


Chukua mwanaume anayetoroka na mwanamke mwingine na kuacha familia yake. Hatambui wakati huo, lakini ameiba kitu kwa kila mtu katika familia yake. Ameiba siku za usoni za mke wake, usalama wake wa kiuchumi, na sifa zake kama mke. Kulingana na maoni ya watoto wake, ameiba Krismasi zao, desturi, usalama wao wa kiuchumi na kihisia, kula pamoja kama familia, na kadhalika.


Sasa, mwanaume aliyefanya haya yote hafikiri kuhusu aliyochukua. Mwanzoni, anafikiria kuhusu alivyofaidi. Lakini mara ya kwanza binti yake mdogo anapomwuliza sababu yake ya kuacha kumpenda mama, moyo wake unavurugwa. Sasa anahisi kuwa ana hatia. Baba ana deni.


Hakuna kitu ambacho kitaondoa mzigo wa hatia kutoka moyo unaohisi hatia ila kulipa deni hilo. Watu wanajaribu kufanya kazi kuondoa, wanatoa huduma, wanatoa mali, ama hata kuomba ili kuondoa. Lakini hakuna kiasi cha matendo mema, huduma kwa jamii, kusaidia maskini kwa kutoa, ama Jumapili nyingi kanisani inayoweza kuondoa hatia. Ni deni. Na lazima ilipwe ama ifutiliwe mbali ili moyo wenye hatia upate tulizo.


Hatia yako itaghairiwa vipi? Jibu lipo katika mstari mmoja ambao nilijifunza kama mtoto: 1 Yohana 1:9. “Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote” (Nen).


Kuungama kuna nguvu ya kuvunja mzunguko wa dhambi. Na kama dawa nyingi, itafaulu ikitumiwa ifaavyo. Matumizi bora ni kwamba tunapoungama, si kwa Mungu pekee, bali pia watu ambao tuliwakosea.


Watu wenye hatia huwa wanaendelea kukosea. Na ikiwa unaendelea kuwa na siri, ikiwa unaendelea kutuliza dhamiri yako kwa kumwomba Mungu msamaha, unapanga kurudia yaliyopita. Ilihali, ukianza kuungama dhambi zako kwa watu ambao uliwakosea, inaelekea kwamba hutarudi na kutenda dhambi hizo tena.


Ungama kwa Mungu na wengine, na utaua adui huyu wa moyo wako.


Mbona unahisi kwamba una hatia? Ungama dhambi zako kwa Mungu na kwa yeyote ambaye ulimkosea. Ifanye leo.


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Enemies Of The Heart

Kama vile moyo unaougua unavyoweza kuangamiza mwili wako, moyo wa kihisia na kiroho unaougua unaweza kukuangamiza pamoja na mahusiano yako. Kwa siku tano zifuatazo, ruhusu Andy Stanley akusaidie kujitazama ndani yako adu...

More

Tungependa kuwashukuru Andy Stanley na Multnomah kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: bit.ly/2gNB92i

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha