Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano

Wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu (Rum 2:4). Dhambi yako itaonekana, na utachukiza namna ambavyo ulimkosea Mungu. Ndivyo Nabii awakumbushavyo Waisraeli. Wakasababisha mataifa yamtukane na kumdharau Mungu, na nchi ikakosa mafanikio. Lakini Bwana anakwenda kufanya upya. Ndipo wote watatambua kuwa Bwana si dhaifu, bali anafanya historia katika Israeli kadri ya makusudi yake. Yerusalemu itajaa watu wakimwadhimisha Bwana. Mungu anafanya haya yote ili mataifa yatambue kuwa yeye ndiye BWANA.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz