Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano

Hii ni simulizi ya Bwana Yesu akiingia Yerusalemu akiwa tayari kuuawa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. Lakini badala ya kuingia kwa simanzi na majonzi, anaingia kwa mvumo wa kishindo cha mfalme. Anatangaza kuwa ni Mfalme mpole, mnyenyekevu asiyejivunia ukuu wake. Kupanda punda kunaashiria unyofu wa moyo wa Mfalme Yesu. Anakuja na amani, na anatawala wote wamwaminio kwa upole. Na wote wanaokubali kuwa raia wake wanatangaziwa wawe wapole na wanyenyekevu. Ndivyo Yesu asemavyo pia katika Mt 5:5, Heri wenye upole; maana hao watairithi nchi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo
