Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano

Bwana Yesu ametumia mitego miwili ya maadui zake kuweka bayana mafundisho mawili muhimu kwa vizazi vyote. Kwanza ni wajibu wa kila raia wa nchi kulipa kodi halali za serikali (Rum 13:1, Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu). Pili mwanadamu anaweza kujenga uhusiano na Mungu wakati akiwa hai duniani. Jambo hili la kujenga uhusiano na Mungu, haliwezekani baada ya kifo. Twaitwa kuweka maisha yetu mikononi mwa Mungu leo, tukiwa bado tuko hai, tuna nguvu na akili timamu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo
