Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano

Gharika ni mfano wa ubatizo. Watu wanane walitoka katika ulimwengu wa uharibifu na kuingia katika ulimwengu mwingine kwa kupitia maji wakiwa ndani ya safina. Vivyo hivyo mtu hutoka katika maisha ya dhambi na kuingia Mbinguni kwa kupitia maji ya ubatizo akiwa ndani ya safina ambayo ni Yesu Kristo! Waovu walizikwa kwa maji. Na watu wanane walipata maisha mapya kwa njia ya safina. Vilevile uovu wetu huzikwa katika ubatizo, na tunafufuliwa kiroho na kupata maisha mapya! Ndivyo tunavyosoma katika 1 Pet 3:18-21, Kristo aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. Na katika Rum 6:3-5, Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo
