Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusikiliza Kutoka Mbinguni: Kusikiliza kwa ajili ya Bwana katika maisha ya kila sikuMfano

Hearing From Heaven: Listening for the Lord in Daily Life

SIKU 5 YA 5

Sauti ya Mbinguni inasema, "Nikimbilie Mimi."

Nilikuwa kijana mdogo nikikua. Na kwa masikitiko, bado ninakua.

Maisha katika makazi duni ya Nairobi mara nyingi yanaambatana na vurugu, na kukosa kwangu mwili mkubwa ni wazi nilikuwa nakumbana na uonevu. Wakati mwingine, nilijisikia kuwa kila mtu na lwake. Wazazi wetu hawakuwa na muda wa kuhakikisha hatuonewi--walikuwa wanafanya kazi kadri walivyoweza ili kupata kipato.

Nikiwa darasa la sita, nilipata wakati mgumu sana wa kuonewa. Kiongozi wa kundi hilo alikuwa ni jitu. Alinionea sana. Mwishoni mwa juma, nilijikuta nimekata tamaa. Lakini nilikwenda kwenye kituo cha Compassion kanisani kwangu, ambapo walizungumza kuhusu Mungu kuwa kimbilio letu. Nikiwa nasikiliza mafundisho haya, upendo wa Bwana ulimwagika kwangu na nafsi yangu maskini ilifarijiwa.

Kituo cha compassion ilikuwa ni mahali ambapo nilikuwa napata amani na usalama. Wafanyakazi walikuwa wakitujali na kutufariji.

Umewahi kujisikia kuogopa? Umewahi kujisikia hauko salama? Umewahi kujisikia huwezi kulinda uhai wako?Tunaweza kukimbilia kwa Mungu wetu kwa sababu ni Mungu mwema. Anasikia vilio vyetu kwa ajili ya usalama. Anatulinda na uovu.

Kama Daudi, unaweza kumuita Mungu. Anaweza kuyalinda maisha yako! Anaweza kukulinda na hatari za dunia hii. Hebu pata muda wa kuwaombea watoto wote duniani wanaoogopa. Waombee kwa ajili ya roho zao na nafsi zao na uombe kwamba Bwana ajifunue kwao kama kimbilio lao. Amen.

Jifunze zaidi kuhusu programu ya Compassion ambayo mwandishi wetu, Njenga, ananukuu, na jinsi unavyoweza saidia kumleta Roho wa Bwana kwa watoto wanaoishi katika umasikini.

Kuhusu Mpango huu

Hearing From Heaven: Listening for the Lord in Daily Life

Bwana yu hai na anatenda leo, na anazungumza kwa kila mtoto wake moja kwa moja. Lakini wakati mwingine, inaweza kuwa vigumu kumwona na kumsikia. Kwa kuangalia safari ya mtu mmoja kuelekea kuelewa sauti ya Mungu katika vitongoji duni vya Nairobi, utajifunza inakuwaje kumsikia na kumfuata.

More

Tunapenda kuwashukuru Compassion International kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: https://www.compassion.com/youversion