Kusikiliza Kutoka Mbinguni: Kusikiliza kwa ajili ya Bwana katika maisha ya kila sikuMfano

Baba Yako wa Mbinguni Anajua Mahitaji Yako Yote.
Kukulia Nairobi ilikuwa ni vigumu, kusema ukweli. Miaka 1990 ilikuwa na mashaka mengi sana. Machafuko yalikuwa kitu cha kawaida na yaliongezeka kutokana na mgawanyiko wa chama tawala kutokana na wengi kutaka demokrasia ya vyama vingi. Na nyakati za machafuko, masikini wanateseka zaidi. Masikini wanategemea vipato vidogo kukidhi mahitaji yao ya kila siku, na mgawanyiko huo uliwafanya masikini kuteseka zaidi.
Matokeo yake, kutoka kwenye umri mdogo, nililazimishwa na mazingira kujifunza jinsi ya kusubiri.
Kunapokuwa hakuna uhakika wa mapato chanya, kusubiri kunaweza kuwa kugumu sana. Baba yangu alikuwa mfanyakazi wa kibarua, kwa hiyo tulitegemea kipato chake cha kila siku kwa mahitaji ya msingi. Kama akipata kazi, tunakula. Kama hakufanikiwa kupata kazi, tulikuwa hatuli.
Baba yangu alitusomea Mathayo 6:25-34 wakati wa ibada ya familia usiku. Alizungumza juu ya umuhimu wa kuweka matumaini yetu kwa Yesu. Maneno yale ya Yesu yalitupa matumaini katikati ya kutokuwa na uhakika wa maisha. Kama familia, tulitulia katika uhakika kwamba Baba yetu wa mbinguni alijua mahitaji yetu yote. Kumjua na kuwa na Yesu ilikuwa inatosha.
Baba yetu wa mbinguni anajua mahitaji yetu yote. Ya ajabu kiasi gani hiyo?Mungu aliyeumba kila kitu ni Mungu huyo huyo ambaye kwa utofauti hukutana na mahitaji yetu.
Ni rahisi kuwa na shaka kwamba atatimiza. Kutatokea nini kama hataweza kutupatia fedha? afya?, familia? Kwa [jaza mahitaji yako] Jifunze kumtumaini Bwana, hata kama una mashaka kiasi gani. Azimia kusoma na kufuata neno la Mungu kila siku unapongoja jibu la Mungu.
Katika kusubiri, tumaini letu huimarika. Kama watoto wa Mungu, tunamngoja Mungu mwaminifu na mwenye upendo apendaye kukutana na mahitaji ya watoto wake. Muombe mwokozi wako: “Mpendwa Bwana, kama mtoto wako, nakuwa na mashaka juu ya maisha yajayo. Lakini leo naweka tumaini langu kwako kwa sababu wewe siku zote ni mwaminifu katika maisha yangu. Amen.”
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Bwana yu hai na anatenda leo, na anazungumza kwa kila mtoto wake moja kwa moja. Lakini wakati mwingine, inaweza kuwa vigumu kumwona na kumsikia. Kwa kuangalia safari ya mtu mmoja kuelekea kuelewa sauti ya Mungu katika vitongoji duni vya Nairobi, utajifunza inakuwaje kumsikia na kumfuata.
More