Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusikiliza Kutoka Mbinguni: Kusikiliza kwa ajili ya Bwana katika maisha ya kila sikuMfano

Hearing From Heaven: Listening for the Lord in Daily Life

SIKU 2 YA 5

“Sema, Bwana, kwa maana Mtumishi Wako Anasikiliza.”

Mungu siku zote amezungumza wazi wazi na watu wake. Kupitia kwa makuhani na manabii alifunua kweli ambayo ilikuwa inatoa uzima kwa wale waliopenda na kumtegemea. Na bado anapenda kuzungumza na watu wake! Lakini kama hatuwezi kuona na kusikia, maisha yetu kama wafuasi wa Kristo yatakuwa hayawezekani.

Unaweza kufikiria neno la Mungu linapokuwa adimu? kwa siku, au miaka, pasipo kusikia kutoka kwa Mungu? Inaonekana ni mbaya bila matumaini. Lakini hicho ndicho kilichotokea kwenye1 Samweli. Wakati watu wa Mungu walitamani kusikia sauti yake, lichagua kujifunua kwa kijana mdogo.

Kijana Samweli alikuwa haijui sauti ya Mungu. Kwa hiyo aliposikia wito, Samweli aliitika kwa njia aliyoijua: alikimbia kwa mshauri wake! Lakini kupitia kwenye hekima ya Eli, Samweli alianza kuelewa ile sauti ni ya nani na ilisikika vipi.

Sauti ya Mungu yaweza kufahamika. Tunachotakiwa ni kusikiliza kwa ajili gani!

Nilisoma hadithi kama kijana mdogo nilipohudhuria kwenye programu ya Compassion International, na nilitiwa moyo sana. Nikiishi katika umaskini wa kutupwa, siku zote nilitaka Mungu ajifunue kwangu katika njia hii kubwa na ya ujasiri. Lakini ningefanya nini kama kweli angejifunua kwangu? Atataka nifanye nini?

Jifunze kusikiliza sauti ya kweli kuliko sauti ya mashaka, kutokuwa na tumaini au kuvunjika moyo. Zoeza masikio yako kusikiliza habari yake njema! Bwana alitupa neno lake kwa njia ya kitabu--soma kweli yake, iliyo kwa ajili yako, katika Biblia. Tafuta mshauri anayejua sauti ya Bwana na jifunze naye. Jiunge na kikundi cha waamini wanaomjua na kumpenda Bwana na wanaweza kukuinua katika kutaka kuijua sauti ya Bwana.

Eli alimfundisha Samweli jinsi ya kuitikia sauti ya Bwana: "Sema, Bwana, kwa maana mtumishi wako anasikiliza." Ni jibu zuri kiasi gani. Tunatakiwa tujibu hivyo hivyo kila mara tunapomsikia akiiongea.

Bwana anataka kujifunua kwa watu wake. Anataka kutuelekeza na kutuongoza. Unaijua sauti ya Mungu? Unatafuta mwongozo kwa hatua zinazofuata katika maisha yako, biashara, elimu, familia na huduma? Kama hayo ndiyo maombi yako, omba nani “Sema, Bwana, kwa maana mtumishi wako anasikiliza.”

Kuhusu Mpango huu

Hearing From Heaven: Listening for the Lord in Daily Life

Bwana yu hai na anatenda leo, na anazungumza kwa kila mtoto wake moja kwa moja. Lakini wakati mwingine, inaweza kuwa vigumu kumwona na kumsikia. Kwa kuangalia safari ya mtu mmoja kuelekea kuelewa sauti ya Mungu katika vitongoji duni vya Nairobi, utajifunza inakuwaje kumsikia na kumfuata.

More

Tunapenda kuwashukuru Compassion International kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: https://www.compassion.com/youversion