Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusikiliza Kutoka Mbinguni: Kusikiliza kwa ajili ya Bwana katika maisha ya kila sikuMfano

Hearing From Heaven: Listening for the Lord in Daily Life

SIKU 3 YA 5

“Mimi Ndiye Amenituma Kwako.”

Nilipokuwa mtoto, nilipenda sana kusikiliza hadithi za Mungu akiwakomboa wana wa Israeli kutoka Misri. Niliona ukweli kwenye hadithi hizi. Nikiishi katika umaskini mkubwa ilionekana kama kuishi kama mtumwa Misri.

Kukulia katika makazi duni ya Nairobi, Kenya kutakufanya umwite Mungu. Utamuomba akukomboe kutoka kwenye umaskini mkubwa ambao familia yako haidhani inaweza kuukwepa. Nikijua Mungu angeweza kusikia kilio changu na kunisaidia kulinifariji--angekuja kunisaidia. Kama mtunga Zaburi, niliweza kulia, "Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu ni katika Bwana, aliyezifanya mbingu na nchi."

Hadithi ya Kutoka ilithibitisha kwamba Mungu alisikia kilio cha muda mrefu cha watu wake na akatafuta njia ya kuwakomboa kwa ajili ya ufalme wake. Na anakuona na wewe, pia.

Zaidi ya hayo, Mungu alimuinua mtu kuwaongoza watu wake kutoka utumwani. Mungu alimhakikishia Musa kwamba atakuwa pamoja naye. "Mimi ndiye amenituma kwako." Musa alitakiwa kusikiliza na kujua aliyekuwa anamuita. Kama waamini, tunahitaji kukumbuka nani aliyetuita katika maisha tunayoishi. Yesu, Mimi ndiye, yuko pamoja nasi. Yeye ndiye anayetuongoza na kutuwezesha kutimiza kazi aliyotuitia kuifanya.

Bwana aliona mateso ya wana wa Israeli huko Misri na alikuja kuwakomboa.

Je unamngoja Bwana? Inaonekana kama milele? Tunamngoja Mungu kwa saburi katika umasikini, magonjwa, utajiri na katika hali zote kwa sababu tunajua anasikia maombi yetu na kuona hali tunazokabiliana nazo.

Kuhusu Mpango huu

Hearing From Heaven: Listening for the Lord in Daily Life

Bwana yu hai na anatenda leo, na anazungumza kwa kila mtoto wake moja kwa moja. Lakini wakati mwingine, inaweza kuwa vigumu kumwona na kumsikia. Kwa kuangalia safari ya mtu mmoja kuelekea kuelewa sauti ya Mungu katika vitongoji duni vya Nairobi, utajifunza inakuwaje kumsikia na kumfuata.

More

Tunapenda kuwashukuru Compassion International kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: https://www.compassion.com/youversion