Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 12Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12

SIKU 23 YA 31

Tumaini la Kikristo kwamba Yesu aja upesi, halitufundishi ulegevu na uzembe ambao tokeo lake ni njaa na kuwasumbua wengine (m.11:Wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine), bali hutufanya tutende kazi kwa utulivu (m.12: Watende kazi kwa utulivu) ili tujipatie chakula na hata uwezo wa kutenda mema (m.12-13:Kula chakula chao wenyewe … ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema). Paulo alishuhudia hiyo kwa mfano wake mwenyewe, akikaa kwao (m.7-9: Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata; kwa sababu hatukuenda bila utaratibu kwenu; wala hatukula chakula kwa mtu ye yote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulitenda kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote. Si kwamba hatuna amri, lakini makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate). Wale wasiotaka kufanya kazi, wasipatiwe chakula, bali waonywe (m. 10 na 12:Ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula … Basi twawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe). Wasipojirekebisha, waumini wasijenge urafiki nao (ni maana ya msizungumze nayekatika m.14), bali wazidi kuonywa ili waone aibu, yaani kutubu (m.14-15:Ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari; lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu).

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12

Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wa...

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha