Soma Biblia Kila Siku 12Mfano

Neno kwa hiyokatika m. 11 linaonyesha kwamba maombezi ya Paulo yatokana na alivyoandika katika 1:5 kwamba Wathesalonike wastahili Ufalme wa Mungu. Mungu aliyewaita wawe watoto wake, mwenyewe atawastahilisha, akiwajaza nia ya kutenda mema. Maana yake si kwamba kazi yao itawastahilisha, maana ni kazi ya imani (m.11: Kwa hiyo twawaombea ninyi sikuzote, ili Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu), yaani waokolewa kwa neema (m.12: Kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo). Angalia kwamba imani hutuunganisha na Yesu namna hii kwamba yeyeanatukuzwa wakati imani yetu katika yeye ikitenda kazi ndani yetu, na sisitutatukuzwa wakati Yesu akija kwa utukufu (m.12:Jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake; ling. Kol 3:4 inayosema, Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

MWANGA Kuvutiwa Maishani Na Mwanga Ajabu Wa Mungu

Kuwa Karibu Na Mungu Kila Siku

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Upendo Wa Bure

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?
