Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 12Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12

SIKU 14 YA 31

Wanadamu wa vizazi vyote watakusanyika mbele za Bwana Yesu siku ya mwisho. Hapo kila mmoja atapokea hukumu yake kutokana na alivyoenenda duniani. Yesu anatuonyesha kuwa matendo ya watu walioenenda kwa usahihi mbele za Mungu yatakuwa yanakumbukwa, hata kama wao walioyatenda watakuwa hawayakumbuki. Angalia kuwa Yesu anawaambia wamemtendea yeye, yaani ni matendo ya imani yao. Watapata heshima kubwa kwa sababu ya hayo. Kumbuka, wokovu ni zawadi ya Mungu kwa waaminio wote, na hatuingii mbinguni kwa matendo mema. Hayo ni wajibu wetu kuyatenda duniani. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo (Efe 2:10).

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12

Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wa...

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha