Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 24 YA 30

Kabla hajawa Mkristo, Paulo alielimika sana katika dini ya Kiyahudi. Kwa hiyo alijua maswali ya udadisi ambayo Wayahudi wangeweza kumwuliza kutokana na mafundisho yake. Kwa hiyo ameamua mwenyewe kuyauliza maswali haya na kuyajibu moja moja. Hii ni mbinu yake ya kuwafundisha Wakristo wa Rumi mambo ya msingi ya imani. Paulo anamlinganisha Myahudina Mtaifa akiuliza swali: Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini?(m.1). Sisitungeweza kumlinganishaMkristona Mtaifa na kujibu kama Paulo: Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu(m.2). Zingatia pia kwamba kuasi kwa Myahudi (au Mkristo) hakumfanyi Mungu kuwa mwongo:Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo(m.3-4)!

Andiko

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mi...

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha