Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 27 YA 30

Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria (m.28). Njia ya kufika kwa Mungu ni moja kwa watu wote, nayo ni njia ya imani. Imani ya kuamini neema ya Mungu kwamba bila ustahili wangu ananisamehe dhambi zote kwa sababu ya upatanisho katika damu ya Yesu Kristo, ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake(m.25). Kwa kuamini haya twashinda katika kesi yetu mbele ya Mungu, yaani, twahesabiwa haki.Mungu ni hakimu na sisi ni washtakiwa. Twastahili hukumu ya kifo, lakini Mungu anatoa hukumu kuwa hatuna dhambi tunapomwamini Yesu, maana Yesu alipigwa na adhabu ya Mungu badala yetu!

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mi...

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha