Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati? (m.23). Paulo anawakemea Wayahudi. Mungu amewapa mwanga wa pekee katika neno lake (torati), mwanga ambao Mataifa hawana:Wewe, ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea torati, … na kuyajua mapenzi yake[Mungu], … nawe umeelimishwa katika torati(m.17-18). Lakini mwanga huu usipowafanya waishi katika imani ya kweli, hautawasaidia lolote. Ndivyo Paulo anavyothibitisha katika m.21-25. Mioyo yao iko mbali na Mungu. Ni wanafiki. Wana alama ya kuwa Wayahudi, lakini wamemwasi Mungu. Yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani (m.29).Zingatia m.26-27: Ikiwa yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! Kutokutahiriwa kwake hakutahesabiwa kuwa kutahiriwa?Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati?Ujumbe: Je, sisi tu Wakristo kweli kwa ndani?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku 12

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila Asubuhi

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku 10

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021
