Uwekezaji Wako Ulio Bora!

Siku1 ya 5 • Usomaji wa leo

Ibada

“Uhakika   wa Mapato!”

Katika   ulimwengu wa leo, sentensi hii inafanya mtu astuke na kuleta kushukiwa. Lakini   kuna sheria inayofanya kazi karibu katika kila eneo la maisha: sheria ya   wakati wa kupanda na kuvuna, au kwa maneno rahisi zaidi, “unavuna ulichopanda.”   

Huwezi   kuvuna mavuno mpaka kwanza upande mbegu. Huwezi kupata  mapato mpaka kwanza ufanye uwekezaji. Huwezi   kupata faida ya bidhaa au huduma mpaka kwanza uinunue. Huwezi kuwa na afya   bila ya kula chakula bora na kufanya mazoezi. Kwa mifano yote hii, mapato yanayopatikana   huendana na ubora wa nguvu iliyotolewa kwanza.

Sheria   hiyo hiyo inafanya kazi katika mahusiano yetu na Mungu. Hatuwezi kuvuna   maisha ya mwendo wa utoshelevu na baraka na Mungu mpaka pale tunapokuwa tumepanda mbegu  zitakazotoa mavuno hayo.   Habari njema ni kwamba Mungu ameweka tayari mbegu njema kwa ajili yetu -   inaitwa  Neno Lake,  Biblia. Kupanda kwa ukarimu neno la Mungu   katika maisha yetu hutuhakikishia mapato tele katika uwekezaji huo.