Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Yesu Mfalme: Ibada ya Pasaka na Timothy KellerMfano

JESUS THE KING: An Easter Devotional By Timothy Keller

SIKU 3 YA 9

“Zaidi ya Uliyotarajia”



Wakati mwingine ninapoenda kwa Yesu, anaruhusu mambo yatendeke ambayo siyaelewi. Matendo yake hayaafikiani na mpango wangu, na sielewi namna yake ya kufanya mambo. Lakini ikiwa Yesu ni Mungu, basi sharti awe na ukuu wa kuwa na sababu nyinginezo za kukuruhusu upitie mambo usiyoyaelewa. Uwezo wake hauna mipaka, tena busara na upendo wake. Maumbile hayakujali, lakini Yesu amejawa upendo usioweza kudhibitiwa kwako. Laiti wanafunzi wangejua kwa kweli kwamba Yesu aliwapenda, ikiwa wangeelewa kwa kweli kwamba alikuwa mwenye nguvu na vilevile mwenye upendo, hawangeogopa. Msingi wao, wa kwamba ikiwa Yesu aliwapenda basi hangeruhusu mambo mabaya yawatendekee, ulikosea. Anaweza kupenda mtu ilhali anaruhusu mambo mabaya yawatendekee, kwa sababu yeye ni Mungu—kwa sababu anajua zaidi yao.



Ikiwa una Mungu ambaye ana ukuu na uwezo zaidi hadi unamkasirikia kwa sababu hajakomesha mateso yako, basi una Mungu ambaye ana ukuu na uwezo unaomruhusu kuwa na sababu ambazo huyaelewi. Sharti ukubali mmoja ama mwingine. Mwalimu wangu Elisabeth Elliot alisema vyema aliposema sentensi hizi mbili fupi: “Mungu ni Mungu, na kwa kuwa yeye ni Mungu, anastahili ibada na utumishi wangu. Ninapata pumziko katika matakwa yake pekee, na matakwa yake sharti ni zaidi ya ninavyoweza kuhesabu, kupima, kusema fikra zangu kuhusu mambo yake." Ikiwa umejipata katika dhoruba, uwezo wake ni mkuu na haikupendi. Utakuwa salama tu katika matakwa ya Mungu. Lakini kwa sababu yeye ni Mungu badala yako, matakwa yake sharti ni zaidi ya unavyoweza kupima, kusema na fikra zako kuhusu mambo yake. Je, Mungu ni salama? “Bila shaka yeye si salama. Nani alisema chochote kuhusu usalama? Lakini yeye ni mwema. Yeye ni Mfalme.”



Je, tunapata amani katika Kristo katika matukio ambayo huwa yanaleta wasiwasi na/au utamaushi vipi? Unangoja Yesu akupe usaidizi wapi katika maishani mwako?



Nukuu kutokwa kwa JESUS THE KING cha Timothy Keller

kuchapishwa kwa mpangilio na Riverhead Books, mshiriki wa kikundi cha Penguin (USA) Kampuni ya Penguin Random House. Haki Miliki © 2011 na Timothy Keller



Na kutoka kwa JESUS THE KING STUDY GUIDE nao Timothy Keller na Spence Shelton, Haki Miliki (c) 2015 na Zondervan, tawi la wachapishaji wa HarperCollins Christian.



siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

JESUS THE KING: An Easter Devotional By Timothy Keller

Mwandishi maarufu wa New York Times na mchungaji mashuhuri Timothy Keller anatuletea mfululizo wa vipindi katika maisha ya Yesu kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Marko. Tunapomakinika katika hadithi hizi, anatuletea u...

More

Vifungu kutoka kwa Riverhead Books, mwanachama wa Penguin Random House, Mwongozo kutoka Harper Collins Christian Publishers. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.penguin.com/book/jesus-the-king-by-timothy-keller/9781594486661 ama http://www.zondervan.com/jesus-the-king-study-guide

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha