Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ibada za kabla ya Pasaka kutoka kwa Biblia Takatifu: MosaicMfano

Devotions for Lent from Holy Bible: Mosaic

SIKU 16 YA 46

Egama Kwangu (Karen Sloan)

"Egama kwangu." Mungu hutupa mwaliko huu mimi na wewe katika kila dakika ya maisha yetu Tunaweza chagua kujibu, "Tafadhali, Mungu, niokoe! Njoo haraka, Mungu, na unisaidie." Lakini kwangu mimi, mtazamo wangu mara nyingi hubakia kwangu mimi mwenyewe. Huwa najipata najihusisha na yale yote nimetimiza au yale yote bado sijatimiza. Naamini kuwa hali ya mambo ni matokeo ya uwezo wangu mwenyewe au dosari ya mapungufu yangu mwenyewe. Wakati maisha ni kunihusu, ninapofushwa kutoka kwa uhalisia wa utegemezi wangu kamili kwa Muumba wangu. Kelele za majivuno na wasiwasi zinafanya wito wa kuegama kwa mikono ya milele usisikike.

Tumeundwa na Mungu tuwe wategemezi. Ni utegemezi wa aina mbili - kwanza, moja kwa moja kumtegemea Mungu na pili, kumtegemea Mungu kupitia wale watu Mungu ameleta maishani mwetu. Uwepo wetu unafaa uwe ule wa ushirikiano na wala sio wa kutengwa.

Yesu alipokuwa anaishi maisha yake duniani kama Mungu na binadamu, aliishi maisha ya mwisho daima akimtegemea Babake; na bado pia alitegemea utoaji wa Babake kupitia binadamu wengine. Mungu alimpatia Yesu maisha ya kibinadamu kupitia Maria. Maria alimbeba Yesu kwanza ndani ya mwili wake kisha kwa mikono zake. Malisho ambayo Maria alikula ndiyo yalikuwa malisho ya kwanza aliyoyapokea. Alimtayarishia mkate wake wa kila siku na kumlea kwa moyo wake wote - akitosheleza mojawapo wa mahitaji ya kina ya nafsi ya binadamu.

Katika utu uzima, Yesu alitegemea jamii kwa ujumla kukamilisha kazi aliyoitwa kufanya. Kijana mdogo alitoa mikate mitano na samaki wawili chakula kilichotumika kuwalisha watu elfu tano. Yesu alimuomba maji mwanamke kisimani - na akategemea neno la mwanamke huyo kuhubiria mji wake mzima wa Samaria, kuwaacha wengi kumuamini. Alipozidiwa na huzuni katika bustani la Gethsemane, Yesu alitafuta faraja kwa Petro, Yakobo na Yohana, hata kama walilala wakati Bwana alipowahitaji sana. Wakati Yesu alipokufa msalabani, Maria alikuwepo na wanawake wengine na Yohana, labda tayari kushika mwili wake mara moja ya mwisho. Yesu aliwaomba wanafunzi wake wamfanyie jambo jingine moja, - kumtunza mama yake (Yohana 19:26-27). Hata kaburi lake Yesu lilikuwa zawadi kutoka kwa mmoja wa wafuasi wake (Mathayo 27:59-60).

Ingawaje Yesu hakukaa katika kaburi zaidi ya siku tatu. Kwa sababu Yule aliyemtegemea zaidi kuliko wengine wote alimfufua kutoka mauti hadi uzima.

Kuna uhuru katika utegemezi. Inatusaidia kila mmoja wetu kukubali hatari tuliyomo. Hatufai tena kujificha katika aibu au katika kujitosheleza sisi wenyewe. Mimi na wewe tunaweza chagua kuagama kwa Baba wetu huku tukiwa katika matukio mbalimbali ya maafa na ya kupendeza, tukiomba, "Tafadhali, Mungu, niokoe! Njoo haraka, Bwana, na unisaidie" (Zaburi 70:1).

Tunaegama kwa kumtegemea Bwana, Tunawategemea walioko karibu nasi, na tunaegama pia watakatifu ambao wamekwenda mbele zetu kwa imani. Miaka elfu moja mia sita iliyopita, kiongozi mmoja wa Kikristo kutoka Ulaya kwa jina John Cassian alichapisha mazungumzo yake na watawa wanaoishi jangwani Mashariki ya Kati. Mtawa mmoja mzee, Isaka, alikuwa ametoa sala hili kutoka Zaburi 70 kwa John Cassian alipowatembelea katika monasteri yao. Kitabu cha John Cassian - na sala la Isaka - vilikuwa na ushawishi hadi hata leo Wakristo wengi kote ulimwenguni huanza wakati wa maombi na maandiko ambayo Isaka alimpa John Cassian. Na katika siku ambazo niko mtulivu wa kutosha kusikia wito, Agama kwangu, mimi, pia hujiunga na kitendo hiki cha sala, shukrani kwa John Cassian, Isaka na wamonaki wenzake.

Andiko

Kuhusu Mpango huu

Devotions for Lent from Holy Bible: Mosaic

Ibada Hii ya kila siku kwa siku 46 kabla ya Pasaka iliyochukuliwa kutoka kwa Biblia Takatifu: Mosaic, inaleta pamoja dondoo, masomo na maandiko kukusaidia kulenga akili yako kwa Kristo. Ikiwa huna uhakika msimu wa kabla ya Pasaka unahusu nini au umekuwa ukijihusisha na msimu huu maisha yako yote, utafurahia masomo ya maandiko na ibada za busara kutoka kwa Wakristo kote ulimwenguni na katika historia. Jiunge nasi na kanisa kote duniani kulenga akili zetu kwake Yesu katika wiki zote za kabla ya Pasaka.

More

Tungependa kushukuru Wachapishaji wa Tyndale House kwa ukarimu wao wa kutoa Ibada za kabla ya Pasaka kutoka kwa Biblia Takatifu: Mosaic Kujifundisha mengi kuhusu Biblia Takatifu: Mosaic tafadhali tembelea: www.tyndale.com/p/holy-bible-mosaic-nlt/9781414322056