Methali 26:1-2
Methali 26:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Heshima apewayo mpumbavu haimfai; ni kama theluji ya kiangazi, au mvua ya wakati wa mavuno. Kama shomoro au mbayuwayu wasiotua, kadhalika laana asiyostahili mtu haimtui.
Methali 26:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno; Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu. Kama shomoro katika kutangatanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpati mtu.
Methali 26:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno; Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu. Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.