Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 26

26
1 # Zab 12:8 Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno;
Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu.
2 # Hes 23:8 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,
Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake;
Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.
3Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda,
Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu.
4 # Isa 36:21 Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;
Usije ukafanana naye.
5Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;
Asije akawa mwenye hekima machoni pake.
6Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu
Hujikata miguu, na kunywa hasara.
7Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu;
Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.
8Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe;
Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu.
9Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi;
Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.
10Fundi stadi hufanyiza vitu vyote;
Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao.
11 # 2 Pet 2:22 Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake;
Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.
12Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe?
Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
13Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani,
Simba yuko katika njia kuu.
14Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake;
Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake.
15Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini;
Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake.
16Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake,
Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu.
17Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake;
Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake.
18Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge,
Na mishale, na mauti;
19 # Efe 5:4 Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake,
Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu?
20Moto hufa kwa kukosa kuni;
Na bila mchongezi fitina hukoma.
21 # 2 Sam 20:1 Kama makaa juu ya makaa yanayowaka,
Na kama kuni juu ya moto;
Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui.
22 # Eze 22:9 Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo.
Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.
23 # Lk 22:48 Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbaya
Ni kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha.
24Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake;
Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake.
25Anenapo maneno mazuri usimsadiki;
Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake.
26Ingawa chuki hufunikizwa kwa hila;
Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko.
27 # Est 7:10 Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe;
Naye abingirishaye jiwe litamrudia.
28 # Mit 13:6 Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi;
Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.

Iliyochaguliwa sasa

Mit 26: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha