Methali 2:16-19
Methali 2:16-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Hekima itakuwezesha kumkwepa mwanamke mwasherati, mwanamke malaya wa maneno matamu; mwanamke amwachaye mwenzi wa ujana wake, na kulisahau agano la Mungu wake. Nyumba yake yaelekea kuzimu, njia zake zinakwenda ahera. Yeyote amwendeaye kamwe harudi, wala hairudii tena njia ya uhai.
Methali 2:16-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ili kuokoka na malaya, Naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake; Amwachaye rafiki wa ujana wake, Na kulisahau agano la Mungu wake. Maana nyumba yake inaelekea mauti, Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu. Katika hao wamwendeao harudi hata mmoja, Wala hawazifikilii njia za uzima.
Methali 2:16-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ili kuokoka na malaya, Naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake; Amwachaye rafiki wa ujana wake, Na kulisahau agano la Mungu wake. Maana nyumba yake inaelekea mauti, Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu. Katika hao wamwendeao harudi hata mmoja, Wala hawazifikilii njia za uzima.
Methali 2:16-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba, kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno ya kushawishi kutenda ubaya, aliyemwacha mwenzi wa ujana wake na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu. Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo na mapito yake kwenye roho za waliokufa. Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi, au kufikia mapito ya uzima.