Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 2

2
Thamani ya Hekima
1Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu,
Na kuyaweka akiba maagizo yangu;
2Hata ukatega sikio lako kusikia hekima,
Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu;
3Naam, ukiita busara,
Na kupaza sauti yako upate ufahamu;
4 # Zab 19:10; Mit 3:14,15; Mt 6:19-21 Ukiutafuta kama fedha,
Na kuutafutia kama hazina iliyositirika;
5Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA,
Na kupata kumjua Mungu.
6 # Lk 21:15; Yn 6:45; Yak 1:5 Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima;
Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;
7 # Zab 84:11 Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili;
Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu;
8 # 1 Sam 2:9; 1 Pet 1:5; Zab 37:23,24,28,31 Apate kuyalinda mapito ya hukumu,
Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake.
9Ndipo utakapofahamu haki na hukumu,
Na adili, na kila njia njema.
10Maana hekima itaingia moyoni mwako,
Na maarifa yatakupendeza nafsi yako;
11 # Mit 6:22 Busara itakulinda;
Ufahamu utakuhifadhi.
12Ili kukuokoa na njia ya uovu,
Na watu wanenao yaliyopotoka;
13 # Yn 3:19; Efe 4:18 Watu waziachao njia za unyofu,
Ili kuziendea njia za giza;
14Wafurahio kutenda mabaya;
Wapendezwao na upotoe wa waovu;
15Waliopotoka katika njia zao;
Walio wakaidi katika mapito yao.
16Ili kuokoka na malaya,
Naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake;
17 # Mal 2:14; Mwa 2:24 Amwachaye rafiki wa ujana wake,
Na kulisahau agano la Mungu wake.
18Maana nyumba yake inaelekea mauti,
Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu.
19 # Mhu 7:26; Ebr 13:4 Katika hao wamwendeao harudi hata mmoja,
Wala hawazifikilii njia za uzima.
20 # Ebr 6:12 Ili upate kwenda katika njia ya watu wema,
Na kuyashika mapito ya wenye haki.
21Maana wanyofu watakaa katika nchi,
Na wakamilifu watadumu ndani yake.
22Bali waovu watatengwa na nchi,
Nao wafanyao hila watang’olewa.

Iliyochaguliwa sasa

Mit 2: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha