Methali 21:1-4
Methali 21:1-4 BHN
Moyo wa mfalme ni kama maji yanayotiririka; Mwenyezi-Mungu, huuongoza popote apendapo. Matendo yote ya mtu ni sawa machoni pake, lakini Mwenyezi-Mungu hupima mioyo. Kutenda mambo mema na ya haki, humpendeza Mwenyezi-Mungu kuliko tambiko. Macho ya kiburi na moyo wa majivuno huonesha wazi dhambi ya waovu.