Methali 21:1-4
Methali 21:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Moyo wa mfalme ni kama maji yanayotiririka; Mwenyezi-Mungu, huuongoza popote apendapo. Matendo yote ya mtu ni sawa machoni pake, lakini Mwenyezi-Mungu hupima mioyo. Kutenda mambo mema na ya haki, humpendeza Mwenyezi-Mungu kuliko tambiko. Macho ya kiburi na moyo wa majivuno huonesha wazi dhambi ya waovu.
Methali 21:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote apendapo. Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo. Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka. Mwenye kiburi na moyo wa majivuno, Taa yake ni dhambi.
Methali 21:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza po pote apendapo. Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo. Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka. Macho yenye kiburi, na moyo wa kutakabari, Hata ukulima wa waovu, ni dhambi.
Methali 21:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Moyo wa mfalme uko katika mkono wa BWANA; huuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo. Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, bali BWANA huupima moyo. Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika zaidi kwa BWANA kuliko dhabihu. Macho ya kudharau na moyo wa kiburi, ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi!