Mithali 21:1-4
Mithali 21:1-4 SRUV
Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote apendapo. Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo. Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka. Mwenye kiburi na moyo wa majivuno, Taa yake ni dhambi.