Methali 12:5-7
Methali 12:5-7 BHN
Mawazo ya mwadilifu ni ya haki; mashauri ya mwovu ni ya udanganyifu. Maneno ya waovu lengo lake ni kuua, lakini maneno ya waadilifu huwaokoa wanaotishwa. Waovu huangamizwa na kutoweka kabisa, lakini jamaa ya waadilifu hudumishwa.