Yoshua 21:20-45
Yoshua 21:20-45 SRUV
Na jamaa za wana wa Kohathi, Walawi, hao wana wengine wa Kohathi waliosalia, wao walikuwa na miji ya kura yao katika kabila la Efraimu. Nao wakawapa Shekemu pamoja na mbuga zake za malisho, katika nchi ya vilima ya Efraimu, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Gezeri pamoja na mbuga zake za malisho; na Kibisaumu pamoja na mbuga zake za malisho, na Beth-horoni pamoja na mbuza zake za malisho, miji minne. Tena katika kabila la Dani Elteke pamoja na mbuga zake za malisho, na Gibethoni pamoja na mbuga zake za malisho; na Aiyaloni pamoja na mbuga zake za malisho, na Gath-rimoni pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. Tena katika hiyo nusu ya kabila la Manase, Taanaki pamoja na mbuga zake za malisho, na Gath-rimoni pamoja na mbuga zake za malisho; miji miwili. Miji yote ya jamaa za wana wa Kohathi waliosalia ilikuwa ni miji kumi, pamoja na mbuga zake za malisho. Tena wana wa Gershoni, katika jamaa za Walawi, waliwapa, katika hiyo nusu ya kabila la Manase, Golani katika Bashani pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Beeshtera pamoja na mbuga zake za malisho; miji miwili. Tena katika kabila la Isakari, Kishioni pamoja na malisho yake, na Daberathi pamoja na mbuga zake za malisho; na Yarmuthi pamoja na mbuga zake za malisho, na Enganimu pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. Tena katika kabila la Asheri, Mishali pamoja na mbuga zake za malisho, na Abdoni pamoja na mbuga zake za malisho; na Helkathi pamoja na mbuga zake za malisho, na Rehobu pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. Tena katika kabila la Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho, na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho; miji mitatu. Miji yote ya Wagershoni kwa kuandama jamaa zao ilikuwa ni miji kumi na mitatu, pamoja na mbuga zake za malisho. Tena jamaa za wana wa Merari, hao Walawi waliosalia, katika kabila la Zabuloni, Yokneamu pamoja na mbuga zake za malisho, na Karta pamoja na mbuga zake za malisho, na Dimna pamoja na mbuga zake za malisho, na Nahalali pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. Tena katika kabila la Reubeni, Bezeri pamoja na mbuga zake za malisho, na Yahasa pamoja na mbuga zake za malisho, na Kedemothi pamoja na mbuga zake za malisho, na Mefaathi pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. Tena katika kabila la Gadi Ramothi katika Gileadi pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Mahanaimu pamoja na mbuga zake za malisho; na Heshboni pamoja na mbuga zake za malisho, na Yazeri pamoja na mbuga zake za malisho; jumla yake miji minne. Miji hiyo yote ilikuwa ni miji ya wana wa Merari kwa kufuata jamaa zao, ni hizo jamaa za Walawi zilizosalia; na kura yao ilikuwa ni miji kumi na miwili. Miji yote ya Walawi iliyokuwa kati ya milki ya wana wa Israeli ilikuwa ni miji arubaini na minane, pamoja na mbuga zake za malisho. Miji hiyo kila mmoja ulikuwa pamoja na mbuga zake za malisho, yaliyouzunguka pande zote; ndivyo ilivyokuwa katika miji hiyo yote. Basi BWANA aliwapa Israeli nchi hiyo yote, ambayo aliapa kwamba atawapa baba zao; nao wakaimiliki, na kukaa humo. Kisha BWANA akawapa raha pande zote, sawasawa na hayo yote aliyokuwa amewaapia baba zao; wala katika adui zao wote hakusimama hata mtu mmoja miongoni mwao mbele zao; yeye BWANA akawatia adui zao wote mikononi mwao. Halikuanguka neno lolote katika jambo lolote lililokuwa ni jema ambalo BWANA alikuwa amelinena katika habari ya nyumba ya Israeli; yalitimia mambo yote.