Yoshua 21:20-45
Yoshua 21:20-45 Biblia Habari Njema (BHN)
Watu waliosalia wa ukoo wa Kohathi, ambao pia ni jamaa za kabila la Lawi walipewa miji katika eneo la kabila la Efraimu. Walipewa Shekemu, mji ambao ulikuwa pia mji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho katika nchi ya milima ya Efraimu, na Gezeri pamoja na mbuga zake za malisho, Kibzaimu pamoja na mbuga zake za malisho na Beth-horoni pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni minne. Katika eneo la kabila la Dani walipewa Elteke pamoja na mbuga zake za malisho, Gibethoni pamoja na mbuga zake za malisho, Aiyaloni pamoja na mbuga zake za malisho na Gath-rimoni pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni minne. Katika eneo la nusu ya kabila la Manase walipewa Taanaki pamoja na mbuga zake za malisho na Gath-rimoni pamoja na malisho yake. Jumla ya miji waliyopewa ni miwili. Basi, miji ambayo walipewa jamaa za Kohathi zilizosalia ilikuwa kumi pamoja na mbuga zao za malisho. Jamaa za Walawi za ukoo wa Gershoni, walipewa miji miwili katika nusu ya eneo la kabila la Manase: Golani, huko Bashani, mji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho, na Beesh-tera pamoja na malisho yake. Katika eneo la kabila la Isakari, walipewa Kishioni pamoja na mbuga zake za malisho, Daberathi pamoja na mbuga zake za malisho, Yarmuthi pamoja na mbuga zake za malisho na En-ganimu pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni minne. Katika eneo la kabila la Asheri walipewa Mishali pamoja na mbuga zake za malisho, Abdoni pamoja na mbuga zake za malisho, Helkathi pamoja na mbuga zake za malisho na Rehobu pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni minne. Katika eneo la kabila la Naftali walipewa Kedeshi, mji wa kukimbilia usalama ulioko huko Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji mitatu. Jumla ya miji ya jamaa mbalimbali za ukoo wa Gershoni ilikuwa kumi na mitatu pamoja na mbuga zao za malisho. Walawi wengine waliobaki, yaani wazawa wa Merari, walipewa miji katika eneo la kabila la Zebuluni. Nayo ni Yokneamu pamoja na mbuga zake za malisho, Karta pamoja na mbuga zake za malisho, Dimna pamoja na mbuga zake za malisho na Nahalali pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji minne. Katika eneo la kabila la Reubeni walipewa Bezeri pamoja na mbuga zake za malisho, Yahazi pamoja na mbuga zake za malisho, Kedemothi pamoja na mbuga zake za malisho na Mefaathi pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji minne. Katika eneo la kabila la Gadi walipewa Ramothi wa Gileadi, mji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho, Mahanaimu pamoja na mbuga zake za malisho, Heshboni pamoja na mbuga zake za malisho na Yazeri pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji minne. Miji yote waliyopewa wazawa wa Merari, yaani jamaa za Walawi zilizobaki, ilikuwa kumi na miwili. Jumla ya miji yote ambayo Walawi walipewa katika maeneo ya Waisraeli ilikuwa arubaini na minane pamoja na mbuga zao za malisho. Kila mmoja kati ya miji hii ulizungukwa na mbuga za malisho. Basi, Mwenyezi-Mungu aliwapa Waisraeli nchi yote ambayo alikuwa amewaahidi wazee wao. Nao wakaimiliki na kuishi humo. Mwenyezi-Mungu akawapa amani kila mahali nchini kama alivyowaapia wazee wao. Hakuna adui yeyote aliyethubutu kuwakabili kwani Mwenyezi-Mungu alikuwa amewatia adui hao mikononi mwao. Hakuna hata ahadi yoyote njema ambayo Mwenyezi-Mungu aliiahidi Israeli ambayo haikutimia. Ahadi zote zilitimia.
Yoshua 21:20-45 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na jamaa za wana wa Kohathi, Walawi, hao wana wengine wa Kohathi waliosalia, wao walikuwa na miji ya kura yao katika kabila la Efraimu. Nao wakawapa Shekemu pamoja na mbuga zake za malisho, katika nchi ya vilima ya Efraimu, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Gezeri pamoja na mbuga zake za malisho; na Kibisaumu pamoja na mbuga zake za malisho, na Beth-horoni pamoja na mbuza zake za malisho, miji minne. Tena katika kabila la Dani Elteke pamoja na mbuga zake za malisho, na Gibethoni pamoja na mbuga zake za malisho; na Aiyaloni pamoja na mbuga zake za malisho, na Gath-rimoni pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. Tena katika hiyo nusu ya kabila la Manase, Taanaki pamoja na mbuga zake za malisho, na Gath-rimoni pamoja na mbuga zake za malisho; miji miwili. Miji yote ya jamaa za wana wa Kohathi waliosalia ilikuwa ni miji kumi, pamoja na mbuga zake za malisho. Tena wana wa Gershoni, katika jamaa za Walawi, waliwapa, katika hiyo nusu ya kabila la Manase, Golani katika Bashani pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Beeshtera pamoja na mbuga zake za malisho; miji miwili. Tena katika kabila la Isakari, Kishioni pamoja na malisho yake, na Daberathi pamoja na mbuga zake za malisho; na Yarmuthi pamoja na mbuga zake za malisho, na Enganimu pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. Tena katika kabila la Asheri, Mishali pamoja na mbuga zake za malisho, na Abdoni pamoja na mbuga zake za malisho; na Helkathi pamoja na mbuga zake za malisho, na Rehobu pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. Tena katika kabila la Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho, na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho; miji mitatu. Miji yote ya Wagershoni kwa kuandama jamaa zao ilikuwa ni miji kumi na mitatu, pamoja na mbuga zake za malisho. Tena jamaa za wana wa Merari, hao Walawi waliosalia, katika kabila la Zabuloni, Yokneamu pamoja na mbuga zake za malisho, na Karta pamoja na mbuga zake za malisho, na Dimna pamoja na mbuga zake za malisho, na Nahalali pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. Tena katika kabila la Reubeni, Bezeri pamoja na mbuga zake za malisho, na Yahasa pamoja na mbuga zake za malisho, na Kedemothi pamoja na mbuga zake za malisho, na Mefaathi pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne. Tena katika kabila la Gadi Ramothi katika Gileadi pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Mahanaimu pamoja na mbuga zake za malisho; na Heshboni pamoja na mbuga zake za malisho, na Yazeri pamoja na mbuga zake za malisho; jumla yake miji minne. Miji hiyo yote ilikuwa ni miji ya wana wa Merari kwa kufuata jamaa zao, ni hizo jamaa za Walawi zilizosalia; na kura yao ilikuwa ni miji kumi na miwili. Miji yote ya Walawi iliyokuwa kati ya milki ya wana wa Israeli ilikuwa ni miji arubaini na minane, pamoja na mbuga zake za malisho. Miji hiyo kila mmoja ulikuwa pamoja na mbuga zake za malisho, yaliyouzunguka pande zote; ndivyo ilivyokuwa katika miji hiyo yote. Basi BWANA aliwapa Israeli nchi hiyo yote, ambayo aliapa kwamba atawapa baba zao; nao wakaimiliki, na kukaa humo. Kisha BWANA akawapa raha pande zote, sawasawa na hayo yote aliyokuwa amewaapia baba zao; wala katika adui zao wote hakusimama hata mtu mmoja miongoni mwao mbele zao; yeye BWANA akawatia adui zao wote mikononi mwao. Halikuanguka neno lolote katika jambo lolote lililokuwa ni jema ambalo BWANA alikuwa amelinena katika habari ya nyumba ya Israeli; yalitimia mambo yote.
Yoshua 21:20-45 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na jamaa za wana wa Kohathi, Walawi, hao wana wengine wa Kohathi waliosalia, wao walikuwa na miji ya kura yao katika kabila ya Efraimu. Nao wakawapa Shekemu pamoja na malisho yake, katika nchi ya vilima ya Efraimu, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Gezeri pamoja na malisho yake; na Kibisaumu pamoja na malisho yake, na Beth-horoni pamoja na malisho yake, miji minne. Tena katika kabila ya Dani Elteke pamoja na malisho yake, na Gibethoni pamoja na malisho yake; na Aiyaloni pamoja na malisho yake, na Gath-rimoni pamoja na malisho yake; miji minne. Tena katika hiyo nusu ya kabila ya Manase, Taanaki pamoja na malisho yake, na Gath-rimoni pamoja na malisho yake; miji miwili. Miji yote ya jamaa za wana wa Kohathi waliosalia ilikuwa ni miji kumi, pamoja na malisho yake. Tena wana wa Gershoni, katika jamaa za Walawi, waliwapa, katika hiyo nusu ya kabila ya Manase, Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Beeshtera pamoja na malisho yake; miji miwili. Tena katika kabila ya Isakari, Kishioni pamoja na malisho yake, na Daberathi pamoja na malisho yake; na Yarmuthi pamoja na malisho yake, na Enganimu pamoja na malisho yake; miji minne. Tena katika kabila ya Asheri, Mishali pamoja na malisho yake, na Abdoni pamoja na malisho yake; na Helkathi pamoja na malisho yake, na Rehobu pamoja na malisho yake; miji minne. Tena katika kabila ya Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na malisho yake, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na malisho yake, na Kartani pamoja na malisho yake; miji mitatu. Miji yote ya Wagershoni kwa kuandama jamaa zao ilikuwa ni miji kumi na mitatu, pamoja na malisho yake. Tena jamaa za wana wa Merari, hao Walawi waliosalia, katika kabila ya Zabuloni, Yokneamu pamoja na malisho yake, na Karta pamoja na malisho yake, na Dimna pamoja na malisho yake, na Nahalali pamoja na malisho yake; miji minne. Tena katika kabila ya Reubeni, Bezeri pamoja na malisho yake, na Yahasa pamoja na malisho yake, na Kedemothi pamoja na malisho yake, na Mefaathi pamoja na malisho yake; miji minne. Tena katika kabila ya Gadi Ramothi katika Gileadi pamoja na malisho yake, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Mahanaimu pamoja na malisho yake; na Heshboni pamoja na malisho yake, na Yazeri pamoja na malisho yake; jumla yake miji minne. Miji hiyo yote ilikuwa ni miji ya wana wa Merari kwa kuandama jamaa zao, ni hizo jamaa za Walawi zilizosalia; na kura yao ilikuwa ni miji kumi na miwili. Miji yote ya Walawi iliyokuwa kati ya milki ya wana wa Israeli ilikuwa ni miji arobaini na minane, pamoja na malisho yake. Miji hiyo kila mmoja ulikuwa pamoja na malisho yake, yaliyouzunguka pande zote; ndivyo ilivyokuwa katika miji hiyo yote. Basi BWANA aliwapa Israeli nchi hiyo yote, ambayo aliapa kwamba atawapa baba zao; nao wakaimiliki, na kukaa mumo. Kisha BWANA akawapa raha pande zote, sawasawa na hayo yote aliyokuwa amewaapia baba zao; wala katika adui zao wote hakusimama hata mtu mmoja miongoni mwao mbele zao; yeye BWANA akawatia adui zao wote mikononi mwao. Halikuanguka neno lo lote katika jambo lo lote lililokuwa ni jema ambalo BWANA alikuwa amelinena katika habari ya nyumba ya Israeli; yalitimia mambo yote.
Yoshua 21:20-45 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Koo nyingine za Wakohathi, ambao pia ni Walawi, walipewa miji kutoka kabila la Efraimu: Katika nchi ya vilima ya Efraimu, walipewa: Shekemu (mji wa makimbilio kwa yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji) na Gezeri, Kibsaimu na Beth-Horoni, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne. Pia kutoka kabila la Dani, wakapokea: Elteke, Gibethoni, Aiyaloni na Gath-Rimoni pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne. Kutoka nusu ya kabila la Manase, wakapokea: Taanaki na Gath-Rimoni pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji miwili. Miji hii kumi, na maeneo ya malisho ya kila mji, ilipewa koo za Wakohathi zilizobaki. Koo za Walawi za Wagershoni walipewa: kutoka nusu ya kabila la Manase: Golani katika Bashani (mji wa makimbilio kwa yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji miwili; kutoka kabila la Isakari, walipewa: Kishioni, Daberathi, Yarmuthi na En-Ganimu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne; kutoka kabila la Asheri, walipewa: Mishali, Abdoni, Helkathi na Rehobu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne. Kutoka kabila la Naftali, walipewa: Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji mitano. Miji yote ya koo za Wagershoni ilikuwa kumi na tatu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji. Koo za Wamerari (Walawi waliobaki) walipewa: kutoka kabila la Zabuloni: Yokneamu, Karta, Dimna na Nahalali, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne; kutoka kabila la Reubeni, walipewa: Bezeri, Yahasa, Kedemothi na Mefaathi, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne; kutoka kabila la Gadi, walipewa: Ramothi katika Gileadi (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa ajili ya mauaji), Mahanaimu, Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne. Miji yote waliyopewa koo za Wamerari, waliokuwa mabaki ya Walawi, ilikuwa ni kumi na mbili. Miji yote ya Walawi katika eneo lililomilikiwa na Waisraeli ilikuwa arobaini na nane, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji. Kila mji kati ya miji hii ulikuwa na maeneo ya malisho kuuzunguka; ndivyo ilivyokuwa kwa miji hii yote. Kwa hiyo BWANA akawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo. BWANA akawapa pumziko kila upande, kama vile alivyokuwa amewaapia baba zao, hakuna hata mmoja wa adui zao aliyeweza kusimama mbele yao, BWANA akawatia adui zao wote mikononi mwao. Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri ya BWANA kwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.