Zab 119:33-35
Zab 119:33-35 SUV
Ee BWANA, unifundishe njia ya amri zako, Nami nitaishika hata mwisho. Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, Naam, nitaitii kwa moyo wangu wote. Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako, Kwa maana nimependezwa nayo.