Zaburi 119:33-35
Zaburi 119:33-35 NENO
Ee Mwenyezi Mungu, nifundishe kuyafuata maagizo yako, nami nitayashika hadi mwisho. Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako na kuitii kwa moyo wangu wote. Niongoze kwenye njia ya amri zako, kwa kuwa huko napata furaha.