1
Mateo 15:18-19
Swahili Roehl Bible 1937
SRB37
Lakini yanayotoka kinywani mwa mtu yametoka moyoni mwake, nayo ndiyo yanayomtia mtu uchafu. Kwani moyoni hutoka mawazo mabaya: uuaji, uzinzi, ugoni, wizi, usingiziaji, matusi.
Linganisha
Chunguza Mateo 15:18-19
2
Mateo 15:11
Kinachoingia kinywani sicho kinachomtia mtu uchafu, ila kinachotoka kinywani ndicho kinachomtia mtu uchafu.
Chunguza Mateo 15:11
3
Mateo 15:8-9
Ukoo huu huniheshimu kwa midomo tu, lakini mioyo yao inanikalia mbali. Hivyo hunicha bure, kwani hufundisha mafundisho yaliyto maagizo ya watu tu.
Chunguza Mateo 15:8-9
4
Mateo 15:28
Ndipo, Yesu alipojibu akimwambia: Mama, umenitegemea kabisa. Na uvipate unavyovitaka! Saa ile ile binti yake akapona.*
Chunguza Mateo 15:28
5
Mateo 15:25-27
Naye mwanamke akaja, akamwangukia, akasema: Bwana, nisaidie! Naye akajibu akisema: Haifai kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia vijibwa. Mwanamke akasema: Ndio Bwana, lakini nao vijibwa hula makombo yanayoanguka mezani pa bwana zao.
Chunguza Mateo 15:25-27
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video