1
Warumi 6:23
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
TKU
Watu wanapotenda dhambi, wanapokea malipo ya dhambi, ambayo ni kifo. Lakini Mungu huwapa watu wake zawadi ya bure, yaani uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Linganisha
Chunguza Warumi 6:23
2
Warumi 6:14
Dhambi haitakuwa mtawala wenu, kwa sababu hamko chini ya sheria. Sasa mnaishi chini ya neema ya Mungu.
Chunguza Warumi 6:14
3
Warumi 6:4
Hivyo, tulipobatizwa, tulizikwa pamoja na Kristo na kushiriki katika kifo chake. Na kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa nguvu ya ajabu ya Baba, ndivyo nasi tunaweza kuishi maisha mapya sasa.
Chunguza Warumi 6:4
4
Warumi 6:13
Msiitoe sehemu ya miili yenu kwa dhambi kwa ajili ya kutumika kutenda maovu. Jitoeni kwa Mungu, kama watu waliokufa lakini walio hai. Toeni sehemu za miili yenu kwa Mungu ili zitumiwe kwa kutenda mema.
Chunguza Warumi 6:13
5
Warumi 6:6
Tunajua kuwa utu wetu wa zamani ulikufa msalabani pamoja naye. Hivyo ndivyo maisha ya utumwa tuliyokuwa nayo yalivyoangamizwa ili tusiendelee kuitumikia dhambi tena.
Chunguza Warumi 6:6
6
Warumi 6:11
Kwa namna hiyo hiyo, mnapaswa kujiona kama mliokufa kwa dhambi na mlio hai kwa nguvu za Mungu kupitia Kristo Yesu.
Chunguza Warumi 6:11
7
Warumi 6:1-2
Hivyo, je, mnadhani inatupasa tuendelee kutenda dhambi ili Mungu atupe neema nyingi zaidi na zaidi? Hapana! Utu wetu wa zamani wa dhambi ulikwisha. Umekufa. Je! tutaendeleaje kuishi katika dhambi?
Chunguza Warumi 6:1-2
8
Warumi 6:16
Hakika mnajua kuwa unakuwa mtumwa wa jambo lolote unaojitoa kulifanya. Chochote au yeyote unayemtii atakuwa bwana wako. Unaweza kufuata dhambi, au kumtii Mungu. Kufuata dhambi kunaleta kifo cha kiroho, lakini kumtii Mungu kunakufanya uhesabiwe na Mungu.
Chunguza Warumi 6:16
9
Warumi 6:17-18
Hapo zamani mlikuwa watumwa wa dhambi na dhambi iliwatawala. Lakini ashukuriwe Mungu, mlitii kwa hiyari mafundisho yote aliyowaelekeza. Mliwekwa huru kutoka katika dhambi, na sasa ninyi ni watumwa wa uaminifu wa wema wa Mungu.
Chunguza Warumi 6:17-18