1
2 Wafalme 2:9
Neno
NEN
Walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, “Niambie, nikufanyie nini kabla sijaondolewa kutoka kwako?” Elisha akajibu, “Naomba nirithi sehemu maradufu ya roho yako.”
Linganisha
Chunguza 2 Wafalme 2:9
2
2 Wafalme 2:11
Walipokuwa wakitembea pamoja na kuzungumza, ghafula gari la farasi la moto na farasi wa moto vilitokea na kuwatenganisha wao wawili, naye Eliya akapanda mbinguni katika upepo wa kisulisuli.
Chunguza 2 Wafalme 2:11
3
2 Wafalme 2:10
Eliya akasema, “Umeomba jambo gumu. Lakini kama utaniona wakati ninapoondolewa kutoka kwako litakuwa lako. La sivyo, hutalipata.”
Chunguza 2 Wafalme 2:10
4
2 Wafalme 2:14
Ndipo akalichukua lile vazi ambalo lilikuwa limeanguka kutoka kwa Eliya, naye akayapiga yale maji nalo. Akauliza, “Yuko wapi sasa BWANA, Mungu wa Eliya?” Elisha alipoyapiga maji, yakagawanyika kulia na kushoto, naye akavuka.
Chunguza 2 Wafalme 2:14
5
2 Wafalme 2:12
Elisha aliliona hili, naye akapaza sauti, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya vita ya Israeli na wapanda farasi wake!” Naye Elisha hakumwona tena. Kisha akaishika nguo yake na kuirarua vipande viwili.
Chunguza 2 Wafalme 2:12
6
2 Wafalme 2:8
Eliya akatoa vazi lake, akalikunja na kupiga maji nalo. Maji yakagawanyika upande wa kuume na upande wa kushoto, nao wawili wakavuka pakavu.
Chunguza 2 Wafalme 2:8
7
2 Wafalme 2:1
BWANA alipokuwa karibu kumchukua Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya na Elisha walikuwa njiani wakitoka Gilgali.
Chunguza 2 Wafalme 2:1