YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

DAY 20 OF 29

Mahali pa kumwabuduMungu panapambwa kwa kutumia uumbaji wa Mungu. Binadamu anashiriki kupamba mahali patakatifu kwa kufuata kanuni maalumu zilizoagizwa na Mungu Mwenyezi. Hema ya kukutania ina taa kwa ajili ya kutoa mwanga. Vyombo vya mahali patakatifu ni vyenye thamani ya juu sana. Ramani ya mahali hapa aliijua Musa peke yake. Kwani ni yeye aliyeipokea baada ya kuonyeshwa na Mungu pale mlimani. Mfano wa ramani hii unatoka kwa Mungu aliye mtakatifu. Tafakari ilivyoandikwa katika Ebr 8:5: Waliotoa sadaka kipindi hichowalitumikia mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu

More