YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Sample

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

DAY 21 OF 30

Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake(m.20). Reubeni na Yuda hawakupenda kumwaga damu ya ndugu yao (m.21-22, 26-27). Hata hivyo hawakuzuia Yusufu kutendewa vibaya. Ila binadamu hawezi kuzuia mpango wa Mungu! Maana kwa njia ya Yusufu kufika Misri ndivyo ndoto alizopewa na Mungu zikatimizwa! Maisha yake ni mfano wa maisha ya Yesu. Yesu naye alitumwa akakataliwa; yaani,walio wake hawakumpokea(Yn 1:11).

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More