YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

DAY 10 OF 30

Yesu alishinda nguvu za dhambi alipotimiza torati, na aliondoa uchungu wa kifo alipokufa na kufufuka kwa ajili ya dhambi zetu. Kwa hiyo atawapa waumini wote kushinda ushindi mkuu atakapokuja mara ya pili. Hapo atauhukumu ulimwengu na kulichukua Kanisa. Mabadiliko yatakayoletwa yatawahusu waumini waliokwisha kufa, Watafufuliwa kimwili. Vilevile yatawahusu waumini watakaokuwa wanaishi bado duniani siku ya mwisho. Hao hawatakufa bali watageuzwa tu katika hali ya utukufu. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele (1 The 4:15-17).