Soma Biblia Kila Siku 10/2020Sample

Hapa mtume Petro hufundisha juu ya ushahidiwa Wakristo, jinsi unavyotakiwa kuonekana katika mwenendo wao. Wametoka tayari katika hali moja (tamaa za kwanza- mwenendo usiofaa) na kuingia katika hali nyingine (watoto wa Mungu - wageni duniani). Kwa hiyo wanapaswa waishi sawasawa na hiyo hali mpya waliyoipata. Wamekuwa watoto wa aliye Mtakatifu kwa hiyo wawe watakatifu kwa mwenendo wao wote! Wamekuwa wenyeji wa Mbinguni kwa hiyo wafikirie na kutumaini sana mambo ya Mbinguni (m.13).
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More