YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

DAY 14 OF 31

Viumbe vyote huonyeshwa utukufu wa Mungu kwa jinsi alivyoviumba na kuviwekea mahali. Hivyo vinamsifu (m.5-6). Kuanzia viumbe vya juu, kama malaika, mpaka wanyama wafugwao, na kuanzia angani hata vilindi vya bahari, BWANA husifiwa. Wanadamu wote wapaswa kumwinua, bila kujali tofauti zao. Wamsifu, si tu kwa sababu ni mwenye mamlaka yote, bali kwa sababu amejijulisha kwao kwa kuwainulia watu wake pembe, yaani, kuwapa wokovu. Kwako Mungu amejijulisha kwa njia ya Yesu. Je, unamsifu na kumwinua?

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More