YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 09/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

DAY 25 OF 30

Siku ya maana sana imefika. Mfalme wa Babeli ameuzingira mji wa Yerusalemu. Nabii anatumia mfano katika m.3-5 wa sufuria litokosalo akimaanisha ukuta wa Yerusalemu kama sufuria na wenyeji wa mji huu kama nyama. Huenda watu wa taifa la Yuda waliobaki ndani ya kuta za Yerusalemu walidhani wako salama, lakini Ezekieli anatabiri kwamba majeshi ya Babeli watawashambulia na kuwaangamiza humohumo ndani. Wapo Wakristo ambao wamejificha kwenye majina ya kuitwa Wakristo, kumbe maisha yao ni ya kipagani. Siku ya hukumu ikifika majina yao wala kanisa havitakuwa msaada kwao. 

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More