1
Marko 4:39-40
Biblia Habari Njema
BHND
Basi, akaamka, akaukemea ule upepo na kuyaamrisha mawimbi ya ziwa, “Kimya! Tulia!” Hapo upepo ukakoma, kukawa shwari kabisa. Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mbona mnaogopa? Je, bado hamna imani?”
ប្រៀបធៀប
រុករក Marko 4:39-40
2
Marko 4:41
Nao wakaogopa sana, wakawa wanaulizana, “Huyu ni nani basi, hata upepo na mawimbi vinamtii?”
រុករក Marko 4:41
3
Marko 4:38
Yesu alikuwa sehemu ya nyuma ya mashua, amelala juu ya mto. Basi, wanafunzi wakamwamsha na kumwambia, “Mwalimu, je, hujali kwamba sisi tunaangamia?”
រុករក Marko 4:38
4
Marko 4:24
Akawaambia pia, “Sikilizeni kwa makini mnachosikia! Kipimo kilekile mnachowapimia watu wengine, ndicho mtakachopimiwa; tena mtazidishiwa.
រុករក Marko 4:24
5
Marko 4:26-27
Yesu akaendelea kusema, “Ufalme wa Mungu ni kama ifuatavyo. Mtu hupanda mbegu shambani. Usiku hulala, mchana yu macho na wakati huo mbegu zinaota na kukua; yeye hajui inavyofanyika.
រុករក Marko 4:26-27
6
Marko 4:23
Mwenye masikio na asikie!”
រុករក Marko 4:23
គេហ៍
ព្រះគម្ពីរ
គម្រោងអាន
វីដេអូ