YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 38

38
Sala katika mateso
(Zaburi ya Daudi ya matoleo)
1Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako;
usiniadhibu kwa ghadhabu yako.
2Mishale yako imenichoma;
mkono wako umenigandamiza.
3Hamna mahali nafuu mwilini mwangu,
kwa sababu umenikasirikia;
hamna penye afya hata mifupani mwangu,
kwa sababu ya dhambi yangu.
4Nimefunikwa kabisa na dhambi zangu,
zinanilemea kama mzigo mzito mno kwangu.
5Madonda yangu yameoza na kunuka,
na hayo ni matokeo ya ujinga wangu.
6Nimepindika mpaka chini na kupondeka;
mchana kutwa nazunguka nikiomboleza.
7Viungo vyangu vimeshambuliwa na homa;
mwilini mwangu hamna nafuu yoyote.
8Nimelegea na kupondekapondeka;
nasononeka kwa kusongwa moyoni.
9Ee Bwana, wewe wajua tazamio langu lote;
kwako hakikufichika kilio changu.
10Moyo wanidunda, nguvu zimeniishia;
hata macho yangu nayo yamekwisha fifia.
11Rafiki na wenzangu wanaepa kuona mateso yangu,
na jamaa zangu wanakaa mbali nami.
12Wanaotaka kuniua wanatega mitego yao;
wanaonitakia niumie wanatishia kuniangamiza.
Mchana kutwa wanafanya mipango dhidi yangu.
13Lakini mimi nimekuwa kama kiziwi, sisikii;
nimekuwa kama bubu asiyeweza kusema kitu.
14Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia,
kama mtu asiye na chochote cha kujitetea.
15Lakini ninakutumainia wewe, ee Mwenyezi-Mungu;
wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, ndiwe utakayenijibu.
16Nakuomba tu maadui wasinisimange,
wasione fahari juu ya kuanguka kwangu.
17Karibu sana nitaanguka;
nakabiliwa na maumivu ya daima.
18Naungama uovu wangu;
dhambi zangu zanisikitisha.
19Maadui zangu hawajambo, wana nguvu;
ni wengi mno hao wanaonichukia bure.
20Hao wanaonilipa maovu kwa wema wangu,
wananipinga kwa sababu natenda mema.
21Usinitupe, ee Mwenyezi-Mungu;
ee Mungu wangu, usikae mbali nami.
22Uje haraka kunisaidia;
ewe Mwenyezi-Mungu, uliye wokovu wangu.

Currently Selected:

Zaburi 38: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy