YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 21

21
Shukrani kwa ushindi
(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi)
1Mfalme ashangilia, ee Mwenyezi-Mungu, kwa nguvu yako,
anafurahi mno kwa msaada uliompa.
2Umemtimizia matakwa ya moyo wake;
wala hukumkatalia ombi lake.
3Umemjia, ukampa baraka nzurinzuri;
umemvika taji ya dhahabu safi kichwani mwake.
4Alikuomba maisha nawe ukampa;
ulimpa maisha marefu milele na milele.
5Kwa msaada wako ametukuka sana;
wewe umemjalia fahari na heshima.
6Wamjalia baraka zako daima;
wamfurahisha kwa kuwako kwako.
7Mfalme anamtumainia Mwenyezi-Mungu;
kwa fadhili za Mungu Mkuu atakuwa salama.
8Mkono wako ewe mfalme utawakamata maadui zako wote;
mkono wako wa kulia utawakamata wanaokuchukia.
9Utakapotokea utawaangamiza kama kwa tanuri ya moto.
Mwenyezi-Mungu atawamaliza kwa hasira yake,
moto utawateketeza kabisa.
10Utawaangamiza wazawa wao kutoka duniani;
watoto wao hawatasalia kati ya binadamu.
11Hata kama wakipanga maovu dhidi yako,
kama wakitunga mipango ya hila,
kamwe hawataweza kufaulu.
12Kwa maana wewe utawatimua mbio,
utawalenga usoni kwa mishale yako.
13Utukuzwe ee Mwenyezi-Mungu kwa sababu ya nguvu yako!
Tutaimba na kuusifu uwezo wako.

Currently Selected:

Zaburi 21: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy