YouVersion Logo
Search Icon

Isaya 64

64
1Laiti ungalizipasua mbingu ukashuka chini,
milima ikakuona na kutetemeka kwa hofu! #64:1 Katika Kiebrania ni 64:11.
2Ingeteketea kama moto uchomavyo kichaka,
kama vile moto uchemshavyo maji.
Njoo upate kuwajulisha maadui zako jina lako
nayo mataifa yatetemeke kwa kuwako kwako!
3Wakati ulipotenda maajabu ambayo hatukutazamia,
ulishuka chini nayo milima ikatetemeka ilipokuona.
4 #64:4 Taz 1Kor 2:9 Tangu kale hakuna aliyepata kuona
wala kusikia kwa masikio yake;
hakuna aliyepata kumwona Mungu aliye kama wewe
atendaye mambo kwa ajili ya wale wanaomtegemea!
5Wewe waja kuwasaidia watendao haki kwa furaha,
wanaokukumbuka na kuzingatia njia zako.
Ulitukasirikia tulipokuwa wenye dhambi;
sisi tumeasi kwa muda mrefu.#64:5 aya ya 5 Kiebrania si dhahiri. Tafsiri ya hapa kufuatana na tafsiri ya Kigiriki.
6Sote tumekuwa kama watu walio najisi;
matendo yetu yote mema ni kama nguo chafu.
Sote tunanyauka kama majani,
uovu wetu watupeperusha kama upepo.
7Hakuna hata mmoja anayekuja kukuomba;
hakuna anayejishughulisha kukutafuta.
Wewe unauficha uso wako mbali nasi,
umetuacha tukumbwe na maovu yetu.
8Hata hivyo, ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni Baba yetu.
Sisi ni kama udongo, wewe ni mfinyanzi.
Sisi sote ni kazi ya mikono yako.
9Usitukasirikie mno, ee Mwenyezi-Mungu,
usiukumbuke uovu wetu daima!
Ukumbuke kwamba sisi sote ni watu wako!
10Miji yako mitakatifu imekuwa nyika;
Siyoni umekuwa mahame,
Yerusalemu umekuwa uharibifu.
11Nyumba yetu takatifu na nzuri,
ambamo wazee wetu walikusifu,
imeteketezwa kwa moto.
Mahali petu pote pazuri pamekuwa magofu.
12Je, kwa hayo yote utajizuia usifanye kitu?
Je, utaendelea kunyamaza tu, ee Mwenyezi-Mungu,
na kututesa kupita kiasi?

Currently Selected:

Isaya 64: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy